Zab 142

Zab 142

Sala ya Ukombozi kutoka kwa Watesi

1Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,[#1 Sam 22:1; 24:3]

Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.

2Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,

Shida yangu nitaitangaza mbele zake.

3Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu;

Katika njia niendayo wamenifichia mtego.

4Utazame mkono wa kuume ukaone,

Kwa maana sina mtu anijuaye.

Makimbilio yamenipotea,

Hakuna wa kunitunza roho.

5BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu,[#Omb 3:24]

Fungu langu katika nchi ya walio hai.

6Ukisikilize kilio changu,[#Zab 116:6; 7:1]

Kwa maana nimedhilika sana.

Uniponye nao wanaonifuatia,

Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.

7Uitoe nafsi yangu kifungoni.[#Zab 34:2; 119:17]

Nipate kulishukuru jina lako.

Wenye haki watanizunguka,

Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania