The chat will start when you send the first message.
1Mbona mataifa wanafanya ghasia,[#Mdo 4:25-26]
Na makabila wanatafakari ubatili?
2Wafalme wa dunia wanajipanga,[#Zab 45:7; Yn 1:41]
Na wakuu wanafanya shauri pamoja,
Juu ya BWANA,
Na juu ya masihi wake,
3Na tuvipasue vifungo vyao,[#Lk 19:14]
Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
4Yeye aketiye mbinguni anacheka,[#Zab 11:4]
Bwana anawafanyia dhihaka.
5Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,
Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.
6Nami nimemweka mfalme wangu
Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
7Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,[#Mdo 13:33; Ebr 1:5; 5:5; Mt 8:29]
Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
8Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,[#Dan 7:13,14; Yn 17:4,5]
Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9Utawaponda kwa fimbo ya chuma,[#Ufu 2:26-27; 12:5; 19:15; Mt 21:44]
Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
10Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili,
Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
11Mtumikieni BWANA kwa kicho,
Shangilieni kwa kutetemeka.
12Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira[#Yn 5:22,23; Yer 17:7; #2:12 Au, Pokeeni mafundisho au, Mbu suni Mwana.]
Nanyi mkapotea njiani,
Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi;
Heri wote wanaomkimbilia.