Zab 32

Zab 32

Shangwe kwa Kusamehewa

1Heri aliyesamehewa dhambi,[#Rum 4:7-8; Zab 85:2]

Na kusitiriwa makosa yake.

2Heri BWANA asiyemhesabia upotovu,[#Law 17:4; Rum 5:13; Yn 1:47; 2 Kor 1:12]

Ambaye rohoni mwake hamna hila.

3Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa

Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.

4Kwa maana mchana na usiku

Mkono wako ulinilemea.

Jasho langu likakauka hata nikawa

Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.

5Nalikujulisha dhambi yangu,[#Mit 28:13; Isa 65:24; Lk 15:18]

Wala sikuuficha upotovu wangu.

Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,

Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.

6Kwa hiyo kila mtu mtauwa[#1 Tim 1:16; Isa 55:6; Yn 7:34]

Akuombe wakati unapopatikana.

Hakika maji makuu yafurikapo,

Hayatamfikia yeye.

7Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso,[#Zab 9:9; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3]

Utanizungusha nyimbo za wokovu.

8Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;[#Isa 48:17]

Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

9Msiwe kama farasi wala nyumbu,

Walio hawana akili.

Kwa matandiko ya lijamu na hatamu

Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.

10Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,[#Mit 13:21; Zab 34:8; Mit 16:20; Yer 17:7]

Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka.

11Mfurahieni BWANA;

Shangilieni, enyi wenye haki

Pigeni vigelegele vya furaha;

Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania