Zab 6

Zab 6

Sala ya Kuponywa Ugonjwa Hatari

1BWANA, usinikemee kwa hasira yako,[#Zab 38:1]

Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.

2BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;[#Hos 6:1]

BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.

3Na nafsi yangu imefadhaika sana;[#Mit 18:14; Mt 26:38]

Na Wewe, BWANA, hata lini?

4BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,

Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

5Maana mautini hapana kumbukumbu lako;[#Zab 30:9]

Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?

6Nimechoka kwa kuugua kwangu;

Kila usiku nakieleza kitanda changu;

Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.

7Jicho langu limeharibika kwa masumbufu,

Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.

8Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;[#Mt 7:23; Lk 13:27]

Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.

9BWANA ameisikia dua yangu;[#Zab 3:4; 31:22; 40:1,2]

BWANA atayatakabali maombi yangu.

10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,

Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania