Zab 73

Zab 73

KITABU CHA TATU

Ombi la kuponywa kutoka kwa Waonevu

1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,

Kwa hao walio safi mioyo yao.

2Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka,

Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.

3Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna,

Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.

4Maana hawana maumivu katika kufa kwao,

Na mwili wao una nguvu.

5Katika taabu ya watu hawamo,

Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.

6Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao,[#Mhu 8:11]

Jeuri huwavika kama nguo.

7Macho yao hutokeza kwa kunenepa,

Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.

8Hudhihaki, husimulia mabaya,[#2 Pet 2:18; Yud 1:16]

Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.

9Wameweka kinywa chao mbinguni,[#Ufu 13:6]

Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.

10Kwa hiyo watu wake hugeuka huko,

Na maji yaliyojaa humezwa nao.

11Nao husema, Mungu ajuaje?[#Ayu 22:13; Zab 94:7]

Yako maarifa kwake aliye juu?

12Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki,

Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.

13Hakika nimejisafisha moyo wangu bure,[#Ayu 21:15; Zab 24:4; Mal 3:14; Ebr 10:19-22]

Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.

14Maana mchana kutwa nimepigwa,

Na kuadhibiwa kila asubuhi.

15Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo;

Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.

16Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo;[#Mhu 8:17]

Ikawa taabu machoni pangu;

17Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu,[#Zab 77:13]

Nikautafakari mwisho wao.

18Hakika Wewe huwaweka penye utelezi,

Huwaangusha mpaka palipoharibika.

19Namna gani wamekuwa ukiwa mara!

Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.

20Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka,

Uondokapo utaidharau sanamu yao.

21Moyo wangu ulipoona uchungu,

Viuno vyangu viliponichoma,

22Nalikuwa kama mjinga, sijui neno;

Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.

23Walakini mimi ni pamoja nawe daima,

Umenishika mkono wa kuume.

24Utaniongoza kwa shauri lako,[#Isa 58:8; Yn 14:3; 2 Kor 5:1]

Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.

25Ni nani niliye naye mbinguni,[#Isa 26:8,9; Hab 3:17,18]

Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.

26Mwili wangu na moyo wangu hupunguka,[#Zab 84:2]

Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu

Na sehemu yangu milele.

27Maana wajitengao nawe watapotea;

Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.

28Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu;[#Ebr 10:22]

Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU,

Niyahubiri matendo yako yote.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania