Zab 79

Zab 79

Ombi la Huruma kwa Yerusalemu

1Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,[#2 Fal 25:8-10; 2 Nya 36:17-19; Yer 26:18; Yer 52:12-14]

Wamelinajisi hekalu lako takatifu.

Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.

2Wameziacha maiti za watumishi wako[#Yer 7:33]

Ziwe chakula cha ndege wa angani.

Na miili ya watauwa wako

Iwe chakula cha wanyama wa nchi.

3Wamemwaga damu yao kama maji[#Ufu 11:9]

Pande zote za Yerusalemu,

Wala hapakuwa na mzishi.

4Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,

Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

5Ee BWANA, hata lini? Utaona hasira milele?[#Kum 29:20; Eze 36:5]

Wivu wako utawaka kama moto?

6Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua,[#Isa 45:4; Zab 53:4]

Na falme za hao wasioliitia jina lako.

7Kwa maana wamemla Yakobo,

Na matuo yake wameyaharibu.

8Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,[#Isa 43:25]

Rehema zako zije kutulaki hima,

Kwa maana tumedhilika sana.

9Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,[#Yos 7:0; Yer 14:7]

Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.

Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,

Kwa ajili ya jina lako.

10Kwa nini mataifa kusema,

Yuko wapi Mungu wao?

Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika

Kijulike kati ya mataifa machoni petu.

11Kuugua kwake aliyefungwa[#Hes 14:17]

Na kuingie mbele zako.

Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako

Uwahifadhi wana wa mauti.

12Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao

Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.

13Na sisi tulio watu wako,[#Isa 43:21]

Na kondoo za malisho yako,

Tutakushukuru milele;

Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania