Zab 95

Zab 95

Mwito wa Kuabudu na Kutii

1Njoni, tumwimbie BWANA,

Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.

2Tuje mbele zake kwa shukrani,

Tumfanyie shangwe kwa zaburi.

3Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,

Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

4Mkononi mwake zimo bonde za dunia,

Hata vilele vya milima ni vyake.

5Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,

Na mikono yake iliumba nchi kavu.

6Njoni, tuabudu, tusujudu,[#1 Fal 8:54; 1 Nya 6:13; Ezr 9:5; Dan 6:10; Lk 22:41; Mdo 7:60; 1 Kor 6:20; Efe 3:14; Ayu 35:10; Isa 54:5; Yn 1:3]

Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

7Kwa maana ndiye Mungu wetu,[#Ebr 3:15; 4:7; Ebr 3:7-11; Ebr 3:7-11; Hes 14:22]

Na sisi tu watu wa malisho yake,

Na kondoo za mkono wake.

Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!

8Msifanye migumu mioyo yenu;[#Kut 17:1-7; Hes 20:2-13]

Kama vile huko Meriba

Kama siku ya Masa jangwani.

9Hapo waliponijaribu baba zenu,

Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

10Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile,[#Ebr 3:10]

Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo,

Hawakuzijua njia zangu.

11Nikaapa kwa hasira yangu[#Hes 14:20-23; Kum 1:34-36; 12:9-10; Ebr 4:3,5]

Wasiingie rahani mwangu.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania