The chat will start when you send the first message.
1Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima;[#1 Tim 6:3; 2 Tim 1:13]
2ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi.[#1 Tim 5:1]
3Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;[#1 Tim 3:11]
4ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
5na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.[#Efe 5:22]
6Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi;
7katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,[#1 Tim 4:12; 1 Pet 5:3]
8na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.[#1 Pet 2:15]
9Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,[#Efe 6:5; 1 Tim 6:1; 1 Pet 2:18]
10wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote.[#Tit 1:3]
11Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;[#Efe 1:4; 1 Yoh 2:16]
13tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;[#1 Kor 1:7; Rum 5:2; Flp 3:20]
14ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.[#Kut 19:5; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Zab 130:8; 1 Pet 2:9; 3:13; Gal 1:4; 1 Tim 2:6; Efe 2:10; Eze 37:23]
15Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.[#1 Tim 4:12]