The chat will start when you send the first message.
1NIJAPOSEMA kwa lugha za wana Adamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upato uvumao.
2Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.
3Tena mkiwagawia maskini mali yangu yote, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4Upendo husubiri, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni,
5haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya;
6haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7hustahimili yote, huamini yote, hutumaini yote, huvumilia yote.
8Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
9Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
10lakini ijapo iliyo kamili, iliyo kwa, sehemu itabatilika.
11Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
12Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.
13Bassi, sasa inabaki imani, tumaini, upendo, hizi tatu; na iliyo kuu katika hizi ni upendo.