The chat will start when you send the first message.
1FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
2Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.
3Na killa mwenye kunitumainia hivi hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
4Killa afanyae dhambi, afanya nasi; kwa kuwa dhambi ni nasi.
5Na mnajua ya kuwa yeye alidhihiri, illi aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake.
6Killa akaae ndani yake batendi dhambi; killa atendae dhambi bakumwona, wala hakumtambua.
7Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;
8afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.
9Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
10Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
11Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;
12si kama Kain alivyokuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Nae alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake ya haki.
13Msistaajabu, ndugu, ulimwengu ukiwachukia.
14Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti.
15Killa amchukiae ndugu yake ni mwuaji: nti mnajua ya kuwa mwuaji bana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
16Hivi tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliweka maisha yake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuweka maisha yetu kwa ajili ya ndugu.
17Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia hii, akamwona ndugu yake yu muhitaji, akamzuilia huruma zake, je! huko ndiko kumpenda Mungu?
18Watoto, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, biali kwa tendo na kweli.
19Hivi tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, na mbele zake tutatuliza mioyo yetu
20katika neno lo lote inalotuhukumu mioyo yetu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu nae anajua yote.
21Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;
22na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
23Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.
24Nae azishikae amri zake hukaa ndani yake, nae ndani yake. Na hivi tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa Roho aliyotupa.