1 Yohana 4

1 Yohana 4

1WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.

2Hivi mwaijua Roho ya Mungu; killa roho iungamayo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.

3Na killa roho isiyoungama kwamba Yesu Kristo amekujii katika mwili, haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya adui wa Kristo ambae mmesikia kwamba yuaja; na sasa amekwisha kuwamo duniani.

4Ninyi, watoto wangu, mwatokana na Mungu: nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.

5Hawo ni wa dunia; kwa biyo wanena ya dunia, dunia ikawasikia.

6Sisi twatokana na Mungu. Yeye anijuae Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Hivi twaijua Roho ya kweli, na roho ya upotevu.

7Wapenzi, tupendane: kwa kuwa pendo ni la Mungu, na killa apendae amezaliwa na Mungu, nae anamjua Mungu.

8Asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni pendo.

9Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye.

10Hili ndilo pendo, si kwamba sisi twalimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akampeleka Mwana wake kuwa kipatanislio kwa dhambi zetu.

11Wapenzi, ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.

12Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.

13Hivi tunafahamu ya kuwa tunakaa ndaui yake, nae ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho yake.

14Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.

15Killa aungamae ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, nae ndani ya Mungu.

16Na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu ndani yetu na kuliamini. Mungu ni pendo, nae akaae katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

17Hivi pendo limekamilishwa kwetu, tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.

18Katika pendo hamua khofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje khofu, kwa maana khofu ina adhabu; na mwenye khofu hakukamilishwa katika pendo.

19Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.

20Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.

21Na amri hii tumepewa nae, ya kwamba yeye ampendae Mungu, ampende na ndugu yake.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania