The chat will start when you send the first message.
1ROHO yanena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani,
2kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru kujiepusha na vyakula ambavyo Mungu aliviumba vopokewe kwa shukrani na walio na imani na wenye kuijua sana kweli.
4Kwa maana killa kiumhe cha Mungu ni kizuri, waki hakuma cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani:
5kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kuomba.
6Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata.
7Bali hadithi za kizee, zisizo za dini, uzikatae.
8Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa.
9Neno hili ni amini, lastahili kukubaliwa na wote.
10Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi katika jambo hili, kwa sababu twamtumaini Mungu aliye hayi aliye mwokozi wa watu wote, khassa wa hao waaminio.
11Uwaagize watu hayo na kuwafundisha hayo.
12Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu.
13Hatta nijapo, fanya bidii katika kusoma na kuonya ua kufundisha.
14Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee.
15Uyatafakari hayo, ukae katika hayo. Kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.
16Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.