2 Wakorintho 6

2 Wakorintho 6

1NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,

2(maana anena,

Wakati uliokubalika nalikusikia,

Siku ya wokofu nilikusaidia;

tazama, sasa ndio wakati uliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokofu).

3Tusiwe kwao la namna yo yote katika jambo lo lote, khuduma yetu isilaumiwe;

4bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,

5kafika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika kazi, katika kukesha, katika kufunga;

6katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki,

7katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,

8kwa utukufu na aibu, kwa kunenwa vibaya na kunenwa vyema; kama wadanganyao, bali watu wa kweli;

9kama wasiojulika, bali wajulikao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hayi; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;

10kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.

11Vinywa vyetu vimewafunukia ninyi, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa.

12Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu.

13Bassi, illi mlipe kadiri ile ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), mkunjuliwe mioyo na ninyi.

14Msifungiwe kongwa pamoja na wasioamini, wasio na tabia kama zenu; kwa maana pana shirika gani kati ya haki na uasi? tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Belial? Au aammiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini? Tena pana mapatano gani ya hekalu ya Mungu na sanama?

16Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17Kwa hiyo

Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana,

Wala msiguse kitu kilicho kichafu.

18Nami nitawakaribisheni,

Nitakuwa Baba kwenu,

Na ninyi mtakuwa kwangu wana na binti,

anena Bwana Mwenyiezi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania