Matendo 22

Matendo 22

1ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa.

2Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza: akanena,

3Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi:

4nikawaudhi watu wa Njia hii kiasi cha kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake.

5Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.

6Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhdhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.

7Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, Saul, Saul, Mbona unaniudhi?

8Nikajibu Wewe nani Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambae wewe unaniudhi.

9Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, wakaingia khofu, illakini hawakuisikia ile sauti.

10Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uende hatta Dameski, na huko utaambiwa khabari za mambo vote yaliyoamriwa uyafanye.

11Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fakhari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikafika Dameski.

12Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.

13Nikamwinulia macho yangu saa ile ile.

14Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua upate kujua mapenzi yake, na kumwona Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.

15Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.

16Bassi sasa, unakawiliani? Simama ubatizwe ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana.

17Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemi, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa katika hali ya rohoni,

18nikamwona akiniambia, Hima, toka katika Yerusalemi upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika khabari zangu.

19Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikwafunga wale wanaokuamini na kuwapiga katika masunagogi yao.

20Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali auawe, nikizitunza nguo zao waliomwua.

21Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.

22Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika inchi, kwa maana haifai aishi.

23Walipokuwa wakipiga kelele na kutupa mavazi yao na kurusharusha mavumbi juu,

24yule jemadari akaamuru aletwe ndani ya ngome, akisema aulizwe khabari zake kwa kupigwa, illi ajue sababu hatta wakampigia kelele namna hii.

25Hatta walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paolo akamwambia akida aliyesimama karibu, Je! ni halali kumpiga mtu Mrumi nae hajahukumiwa bado?

26Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? kwa maana mtu huyu ni Mrumi.

27Jemadari akaja, akamwambia, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndio.

28Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa ras-il-mali nyingi. Paolo akasema, Na mimi nalizaliwa katika hali hiyo.

29Bassi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari nae akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.

30Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania