The chat will start when you send the first message.
1PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu;
2Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwaua Yesu Kristo.
3Atukuzwe Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo;
4kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tuwe watakatifu, wasio khatiya mbele zake, katika pendo.
5Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,
6illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:
7Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;
8aliyotuzidishia katika hekima yote na ujuzi;
9akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,
10ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:
11ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;
12illi sisi tuwe sifa ya utukufu wake, tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu;
13katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake,
14aliye arabuni ya urithi wetu, hatta ukombozi wa milki yake Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.
15Kwa sababu hiyo na mimi, tangu nilipopata khabari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,
16siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu;
17Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye:
18macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,
19na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio, jinsi ulivyo, kwa kadiri ya kazi ya nguvu zake hodari,
20aliyotenda katika Kristo alipomfufua, akamweka mkono wake wa kuume katika mbingu,
21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na killa jina litajwalo, si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao nao;
22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajiii ya kanisa,
23lililo mwili wake, ukamilifu wake akamilishae vitu vyote katika vyote.