Waefeso 3

Waefeso 3

1KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—

2ikiwa mmesikia khabari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;

3ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,

4kwa hayo, myasomapo, mtaweza kutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo;

5ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho;

6ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili;

7ambayo nilifanywa mkhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema yake Mungu niliyopewa kwa kadiri ya kutenda kazi kwa uweza wake.

8Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;

9na kuwaangaza watu wote, wajue khabari ya kuishiriki siri ile, ambayo tangu zamani zote ilisetirika katika Mungu, aliyeviumba vyote kwa Yesu Kristo:

10illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni;

11kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.

12Katika yeye tuna ajasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya imani yake.

13Bassi naomba, msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, yaliyo utukufu kwenu.

14Kwa hiyo nampigia magoti Baba,

15ambae kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unakwitwa,

16awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho yake, katika mtu wa ndani;

17Kristo akae mioyoni mwemi kwa imani; illi ninyi, mkiwa na mizizi na misingi katika upendo,

18mpale kufahamu pamoja na watakatifu wofe, mapana na marefu na kwenda juu na kwenda chini;

19na kimjua upendo wake Kristo, ambao hauwezi kufahamiwa vema kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

20Bassi, kwake yeye awezae kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuombayo au tuwazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu,

21kwake yeye utukufu katika Kanisa, na katika Kristo Yesu hatta vizazi vyote vya milele na milele. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania