The chat will start when you send the first message.
1KIISHA, baada va miaka kumi na minane, nalipanda kwenda Yerusalemi pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami.
2Nami nalikwenda kwa kufunuliwa, nikawaeleza injili ile niikhubirivyo katika mataifa, lakini kwa faraglia kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio burre au nalipiga mbio burre.
3Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa:
4bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri.
5Hao waliingia kwa siri wapate kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Yesu Kristo illi watutie utumwani: ambao hatta saa moja hatukujitia chini yao, illi kweli ya Injili ikae pamoja nanyi.
6Lakini wale wenye sifa kwamba wana cheo, walivyo vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwana Adamu—nasema, wale wenye sifa hawakuniongezea kitu,
7bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili va wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa
8(maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha kwenda kwa mataifa);
9tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
10illa neno moja walitutakia, tuwakumbuke maskini; na neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.
11Lakini Petro alipokuja Antiokia, nalishindana nae uso kwa uso, kwa sababu amepasiwa hukumu;
12kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikula pamoja na watu wa mataifa, illakini walipokuja akarudi nyuma akajitenga, akiwaogopa waliotahiriwa.
13Na Wayahudi wakajigeuza pamoja nae, hatta Barnaba nae akachukuliwa na unafiki wao.
14Lakini, nilipoona ya kuwa njia yao haikwenda sawa sawa na kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya watu wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha mataifa kufuata desturi za Wayahudi?
15Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wenye dhambi wa mataifa,
16tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.
17Lakini kama sisi wenyewe tulipokuwa tukitafuta kufanyiziwa wema katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha.
18Maana nikiyajenga tena yale niliyoyabomoa, naonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ui mkosaji.
19Maana mimi kwa sharia naliifia sharia illi nimwishie Mungu.
20Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
21Siibatili neema ya Munga. Maana, ikiwa haki hupatikana kwa sharia, bassi, Kristo alikufa burre.