The chat will start when you send the first message.
1BASSI hatta agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidumia.
2Maana khema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na taa, na meza, na mikate iliyotolewa kwa Mungu; palipoitwa, Patakatifu.
3Na nyuma ya pazia la pili, ile khema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,
4yenye cheteso cha dhahabu, na sanduku ya agano iliyofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye manna, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya agano;
5na juu yake makerubi ya utakatifu, yakilitia kivuli kao la rehema; bassi hatuma nafasi ya kueleza khabari za vitu hivi moja moja.
6Bassi, vitu hivi vikiislia kutengenezwa hivyo, makuhani huingia khema ya kwanza siku zote, wakiyatimiza mambo va ibada.
7Lakini katika khema ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, marra moja killa mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na dhambi za ujinga za watu.
8Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo khema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama.
9Hii ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhahihu zinatolewa, zisizoweza kumkamilisha mtu aabunduye dhamiri yake,
10kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hatta wakati wa matengenezo mapya.
11Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,
12wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
13Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ngʼombe waliyonyunyizwa wenye uchafu hutakasa hatta kuutakatisha mwili;
14bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?
15Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
16Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.
17Kwa maana agano lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, maadam yu hayi yeye aliyelifanya.
18Kwa hiyo hatta lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu.
19Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,
20akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.
21Na ile khema na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivi hivi.
22Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
23Bassi sharti manukulu ya mambo yaliyo mbinguni yasafishwe kwa haya, lakini mambo ya mbinguni yenyewe kwa dhabibu zilizo bora kuliko haya.
24Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;
25wala si kusudi ajitoe marra nyiugi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo patakatifu killa mwaka kwa damu isiyo yake;
26kana ni hivyo, ingalimpasa kuteswa marra nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; lakini sasa, marra moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana, atangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.
27Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu:
28kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.