The chat will start when you send the first message.
1YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,
2Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3mkifahamu ya kuwa kujaribiwa imani yenu huleta saburi.
4Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno.
5Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa.
6Illa aombe kwa imani, pasipo shaka lo lote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa kwa upepo, na kupeperushwa huko na huko.
7Maana mtu yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana;
8mtu wa nia mbili asitasita katika njia zake zote.
9Lakini ndugu asiye na cheo afurahi kwa kuwa ametukuzwa;
10na tajiri kwa kuwa ameshushwa: kwa maana kama ua la majani atatoweka.
11Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; na lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo nae tajiri atanyauka katika njia zake.
12Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
13Mtu, ajarihiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu: maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
14Lakini killa mmoja hujaribiwa akivutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe.
15Khalafu ile tamaa ikiisha kuchuikua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
16Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi.
17Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
18Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.
19Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;
20kwa maana ghadhabu ya mwana Adamu haiitendi haki ya Mungu.
21Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, kapokeeni kwa upole neno lililopandwa, liwezalo kuokoa roho zenu.
22Mwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu.
23Kwa sababu mtu akiwa msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyu ni kama mtu anaejiangalia uso wake wa asili katika kioo.
24Maana hujiangalia, kiisha huendazake, marra akasahau jinsi alivyo.
25Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake.
26Mtu akidhani ya kuwa ana dini, nae hazuii ulimi wake kwa khatamu, akijidanganya moyo wake, dini yake mtu yule haifai.
27Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.