The chat will start when you send the first message.
1Kwa hakika sina haja ya kuwaandikia ninyi juu ya msaada huu kwa watu wa Mungu.
2Ninajua kuwa mnataka kusaidia. Nimekuwa ninajisifu sana juu yenu kwa watu wa Makedonia. Niliwaeleza kwamba ninyi watu wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana. Na shauku yenu ya kutoa zaidi imewafanya watu walio wengi zaidi hapa wawe tayari kutoa pia.
3Lakini ninawatuma kaka hawa kwenu. Sipendi kujisifia kwetu juu yenu kuthibitishwe kuwa ni batili. Nataka muwe tayari kama ambavyo nimesema kuwa mtakuwa tayari.
4Ikiwa baadhi ya Wamakedonia walio wengi wangefuatana nami na kuwakuta hamko tayari, tutaaibika. Tutaibika kwa kuwa tulikuwa na uhakika sana juu yenu. Na ninyi mtaaibika pia!
5Hivyo nikafikiri kuwa niwaombe ndugu hawa waje kwenu kabla ya mimi kuja. Wao watasaidia kufanya maandalizi mapema kwa ajili ya sadaka yenu yenye ukarimu mliyoahidi. Kisha sadaka hii itakuwa tayari tutakapokuja, na itaonekana kuwa baraka, na si kitu kidogo ambacho hamkutaka kutoa.
6Kumbukeni hili: Yeye apandaye mbegu chache atapata mavuno kidogo. Lakini apandaye kwa wingi atapata mavuno mengi.
7Kila mmoja wenu atoe kama alivyo kusudia kutoa katika moyo wake. Hampaswi kutoa ikiwa mnajisia huzuni kufanya hivyo au ikiwa mnasikia kulazimishwa kutoa. Mungu anawapenda wale wanaotoa kwa furaha.
8Na Mungu anaweza kuwapeni baraka zaidi kuliko mlivyo katika kuhitaji kwenu, na daima mtakuwa na kila kitu mnachokihitaji. Mtakuwa na vingi vya ziada vya kutoa kwa kila kazi njema.
9Kama Maandiko yanavyosema,
“Hawakuwa na choyo waliwapa maskini.
Mambo mema waliyoyafanya yatadumu millele.”
10Mungu ndiye huwapa mbegu wale wanaopanda, na anatoa mkate kuwa chakula. Na Mungu atawapeni “mbegu” na kuifanya ile mbegu ikue. Atazalisha mazao makubwa kutokana na wema wenu.
11Mungu atawatajirisha katika namna zote ili mweze kutoa kwa uhuru kila mara. Na kutoa kwenu kulikosimamiwa na sisi kutawafanya watu wamshukuru Mungu.
12Huduma mnayoitoa inawasaidia watu wa Mungu katika mahitaji yao, lakini si hayo tu itendayo. Inaleta pia shukrani nyingi zaidi na zaidi kwa Mungu.
13Huduma hii ni uthibitisho wa imani yenu, na watu watamsifu Mungu kwa sababu kwa uhuru mlitoa mkawapa sehemu pamoja na watu wengine pia. Watamsifu Mungu kwa sababu wanaona jinsi mnavyoifuata injili ya Yesu Kristo ambayo mliipokea kwa wazi kabisa.
14Na wanapoomba kwa ajili yenu, watatamani wangekuwa pamoja nanyi. Watajisikia hivi kwa sababu ya neema ya ajabu aliyowapa Mungu.
15Mungu apewe shukrani kwa kipawa chake ambacho ni ajabu sana kukielezea.