The chat will start when you send the first message.
1Nilifurahi waliponiambia:
“Twende nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.”
2Sasa tuko tumesimama,
kwenye malango yako, ee Yerusalemu!
3Yerusalemu, mji uliojengwa,
ili jumuiya ikutane humo.
4Humo ndimo makabila yanamofika,
naam, makabila ya Israeli,
kumshukuru Mwenyezi-Mungu kama alivyoagiza.
5Humo mmewekwa mahakama ya hukumu ya haki,
mahakama ya ukoo wa kifalme wa Daudi.
6Uombeeni Yerusalemu amani:
“Wote wakupendao na wafanikiwe!
7Ndani ya kuta zako kuwe na amani,
majumbani mwako kuweko usalama!”
8Kwa ajili ya jamaa na ndugu zangu,
ee Yerusalemu, nakutakia amani!
9Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,
ninakuombea upate fanaka!