The chat will start when you send the first message.
1Hii ndiyo migawanyo ya wazao wa Haruni:
Haruni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
2Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.
3Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Haruni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.
4Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.
5Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.
6Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
7Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,
ya pili Yedaya,
8ya tatu Harimu,
ya nne Seorimu,
9ya tano Malkiya,
ya sita Miyamini,
10ya saba Hakosi,
ya nane Abiya,
11ya tisa Yeshua,
ya kumi Shekania,
12ya kumi na moja Eliashibu,
ya kumi na mbili Yakimu,
13ya kumi na tatu Hupa,
ya kumi na nne Yeshebeabu,
14ya kumi na tano Bilga,
ya kumi na sita Imeri,
15ya kumi na saba Heziri,
ya kumi na nane Hapisesi,
16ya kumi na tisa Pethahia,
ya ishirini Yehezkeli,
17ya ishirini na moja Yakini,
ya ishirini na mbili Gamuli,
18ya ishirini na tatu Delaya,
ya ishirini na nne Maazia.
19Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana , kulingana na masharti waliyoelekezwa na Haruni baba yao, kama Bwana , Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;
21Kuhusu Rehabia, kutoka kwa wanawe: Ishia alikuwa wa kwanza.
22Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomothi,
23Wana wa Hebroni:
24Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;
25Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;
26Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.
27Wana wa Merari:
28Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.
29Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi alikuwa Yerameeli.
30Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.
31Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Haruni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.