Yoshua 21

Yoshua 21

Miji kwa Walawi

1Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli

2huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwana aliamuru kupitia Musa kuwa mtupe miji ya kuishi yenye maeneo ya malisho kwa mifugo yetu.”

4Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, kufuatana na koo zao. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Haruni walipewa miji kumi na tatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.

5Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.

6Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na tatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.

7Wazao wa Merari, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na mbili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

9Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina

10(miji hii walipewa wazao wa Haruni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

17Kutoka kabila la Benyamini wakawapa

21Katika nchi ya vilima ya Efraimu, walipewa:

23Pia kutoka kabila la Dani, wakapokea:

25Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea:

kutoka nusu ya kabila la Manase:

28kutoka kabila la Isakari, walipewa:

30kutoka kabila la Asheri, walipewa:

32Kutoka kabila la Naftali, walipewa:

kutoka kabila la Zabuloni:

36kutoka kabila la Reubeni, walipewa:

38kutoka kabila la Gadi, walipewa:

43Kwa hiyo Bwana akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo.

44Bwana akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao.

45Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.