The chat will start when you send the first message.
1Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote.
2Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha;
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema
na fadhili zake zadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.