The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaa
katika Hekalu lako?
Nani awezaye kuishi
katika mlima wako mtakatifu?
2Ni yule aendaye pasipo mawaa,
atendaye yaliyo haki,
asemaye kweli toka moyoni mwake,
3na hana masingizio ulimini mwake,
asiyemtenda jirani yake vibaya,
na asiyemsingizia mwenzake,
4ambaye humdharau mtu mbaya,
lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu,
yule atunzaye kiapo chake
hata kama anaumia.
5Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,
na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.
Mtu afanyaye haya
kamwe hatatikisika.