Ezra 2

Ezra 2

Watu waliorudi kutoka uhamishoni

1Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;[#Ezr 5:8; 6:2; Est 1:1; 8:9; 2 Fal 24:14-16; 2 Nya 36:20]

2ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya watu wa Israeli;

3wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.

4Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.

5Wazawa wa Ara, mia saba sabini na watano.[#Neh 6:18]

6Wana wa Pahath-Moabu, wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili.

7Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

8Wana wa Zatu, mia tisa arobaini na watano.

9Wana wa Zakai, mia saba na sitini.

10Wana wa Binui, mia sita arobaini na wawili.

11Wana wa Bebai, mia sita ishirini na watatu.

12Wana wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili.

13Wazawa wa Adonikamu, mia sita sitini na sita.[#Ezr 7:18; 8:13]

14Wana wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita.

15Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne.

16Wana wa Ateri, wana wa Hezekia, tisini na wanane.

17Wana wa Besai, mia tatu ishirini na watatu.

18Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.

19Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu.

20Watu wa Gibari, tisini na watano.[#Yos 9:17; 2 Sam 21:2]

21Watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu.[#Mwa 35:19; Mt 2:6; Rut 1:19; 1 Nya 2:51]

22Watu wa Netofa, hamsini na sita.

23Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane.

24Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili.

25Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu.

26Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja.[#Yos 18:25; 1 Sam 7:17; 15:34; Yer 31:15]

27Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili.

28Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu.

29Watu wa Nebo, hamsini na wawili.

30Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita.

31Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.[#Ezr 2:7]

32Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini.

33Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano.

34Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano.[#Kum 34:3; 2 Nya 28:15]

35Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini.

36Makuhani; wana wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu.[#1 Nya 9:10; 24:7]

37Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.[#1 Nya 24:14; Ezr 10:20]

38Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba.[#1 Nya 9:12; Ezr 10:22]

39Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.[#1 Nya 24:8]

40Walawi; wana wa Yeshua, wana wa Kadmieli wana wa Hodavia, sabini na wanne.[#Ezr 3:9]

41Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane.

42Akina bawabu; wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na tisa.

43Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi;[#1 Nya 9:2; #2:43 Watumishi hekaluni waliowasaidia Walawi kazi.]

44wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni;

45wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Akubu;

46wana wa Hagabu, wana wa Salmai, wana wa Hanani;

47wana wa Gideli, wana wa Gahari, wana wa Reaya;

48wana wa Resini, wana wa Nekoda, wana wa Gazamu;

49wana wa Uza, wana wa Pasea, wana wa Besai;

50wana wa Asna, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu;

51wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri;

52wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha;

53wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema;

54wana wa Nesia, wana wa Hatifa.

55Wazawa wa watumishi wa Sulemani; wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda;[#1 Fal 9:21]

56wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli;

57wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.

58Wanethini wote, pamoja na wana wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.[#Yos 9:21,27; 1 Nya 9:2; Ezr 7:7; 1 Fal 9:21]

59Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha koo za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;

60wana wa Delaya, wana wa Tobia na wana wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili.

61Tena wa makuhani; wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.[#1 Fal 2:7]

62Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.[#Hes 3:10]

63Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.[#Neh 8:9; Law 22:2,10,15,16; Hes 18:9-11; Kut 28:30; #2:63 ni jina la heshima aliloitwa mtawala.]

64Basi hilo kusanyiko lote nzima, jumla yake ilikuwa watu elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini,[#Isa 10:22]

65tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.

66Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arobaini na watano;

67ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda wao elfu sita, mia saba na ishirini.

68Na baadhi ya wakuu wa koo za baba zao, hapo walipoifikia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake;[#Kut 25:2]

69wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu sitini na moja, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani.[#2:69 ni sarafu, thamani yake ni kama shilingi 21.; #2:69 Mane ya fedha ni kama shilingi 136.]

70Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania