Nehemia 11

Wenyeji wa Yerusalemu na wa nchi ya Yuda.

1Wakuu wa watu wakaja kukaa Yerusalemu, lakini watu wengine wakapiga kura, katika kila watu kumi wapate mmoja wa kumpeleka kukaa Yerusalemu ulio mji mtakatifu; wale wengine tisa wakae mijini.[#Neh. 7:5.]

2Watu wakawabariki hao waume waliojipa mioyo ya kukaa Yerusalemu.

(3-19: 1 Mambo 9:2-17.)

3Hawa ndio wakuu wa mitaa waliokaa Yerusalemu namo mijini mwa nchi ya Yuda; wakakaa kila mtu mahali palipokuwa mali yake katika miji yao: Waisiraeli, watambikaji, Walawi, watumishi wa Nyumbani mwa Mungu na wana wa watumwa wa Salomo.[#Neh. 7:57.]

4Yerusalemu wakakaa wengine wao wana wa Yuda na wana wa Benyamini. Wana wa Yuda walikuwa: Ataya, mwana wa uzia, mwana wa Zakaria, mwana wa Amaria, mwana wa Sefatia, mwana wa Mahalaleli wa wana wa Peresi.

5Na Masea, mwana wa Baruku, mwana wa Koli-Hoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zakaria, mwana wa Msiloni.

6Wana wote wa Peresi waliokaa Yerusalemu walikuwa waume wenye nguvu 468.

7Hawa ndio wana wa Benyamini: Salu, mwana wa Mesulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Masea, mwana wa Itieli, mwana wa Yesaya,

8nyuma yake Gabai-Salai; ni watu 928.

9Yoeli, mwana wa Zikiri, alikuwa msimamizi wao, naye Yuda, mwana wa Hasenua, alikuwa msimamizi wa pili wa mji.

10Watambikaji walikuwa: Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini,

11Seraya, mwana wa Hilkia, mwana wa Mesulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayoti, mwana wa Ahitubu, aliyekuwa msimamizi mkuu wa Nyumba ya Mungu;

12pamoja na ndugu zao walioifanyia Nyumba ya Mungu kazi, walikuwa watu 822. Tena Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amusi, mwana wa Zakaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkia;

13pamoja na ndugu zake walio wakuu wa milango walikuwa watu 242. Tena Amasai, mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Mesilemoti, mwana wa Imeri;

14pamoja na ndugu zao waliokuwa wenye nguvu walikuwa watu 128; msimamizi wao alikuwa Zabudieli, mwana wa Hagedolimu.

15Walawi walikuwa: Semaya, mwana wa Hasubu, mwana wa Azirikamu, mwana wa Hasabia, mwana wa Buni,

16na Sabutai na Yozabadi waliokuwa wenye kazi za nje ya Nyumba ya Mungu, nao waliokuwa miongoni mwao wakuu wa Walawi.

17Tena Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zabudi, mwana wa Asafu, kiongozi wao walioimba shangilio la kushukuru, watu walipoomba. Tena Bakibukia aliyekuwa miongoni mwa ndugu zake; tena abuda, mwana wa samua, mwana wa Galali, mwana wa Yedutuni.

18Walawi wote katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.

19Walinda malango walikuwa: Akubu na Talmoni na ndugu zao; ndio walioyangoja malango, walikuwa watu 172.

20Waisiraeli wengine, nao watambikaji na Walawi wakakaa katika miji yote ya nchi ya Yuda, kila hapo palipokuwa fungu lake.

21Lakini watumishi wa Nyumbani mwa Mungu wakakaa Ofeli; Siha na Gisipa walikuwa wasimamizi wao watumishi wa Nyumbani mwa Mungu.

22Msimamizi wa Walawi mle Yerusalemu alikuwa Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hasabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika wa wana wa Asafu waliokuwa waimbaji, akawasaidia kutumikia Nyumbani mwa Mungu.

23Kwani mfalme aliagiza kazi zao na mshahara wao hao waimbaji, ndio waupate siku kwa siku.

24Petaya, mwana wa Mesezabeli, wa wana wa zera, mwana wa Yuda, alikuwa amewekwa na mfalme kuyatengeneza mambo yote ya watu.

25Nako mashambani kwenye viwanja vya kale wakakaa Wayuda wengine Kiriati-Arba na katika vijiji vyake, tena Diboni na katika vijiji vyake na Yekabuseli na katika viwanja vyake,[#Yos. 20:7; 21:11.]

26tena Yesua na Molada na Beti-Peleti,

27Hasari-Suali na Beri-Seba na katika vijiji vyake,

28Siklagi na Mekona na katika vijiji vyake,[#Yos. 15:31.]

29Eni-Rimoni na Sora na Yarmuti,

30Zanoa, Adulamu na katika viwanja vyao. Lakisi na mashambani kwake, Azeka na katika vijiji vyake; basi, wakatua toka Beri-Seba hata bonde la Hinomu.

31Lakini wana wa Benyamini wakakaa kuanzia Geba: Mikimasi na Aya na Beteli na katika vijiji vyake,[#Yos. 18:22.]

32Anatoti, Nobu, Anania,

33Hasori, Rama, Gitaimu,

34Hadidi, Seboimu, Nebalati,

35Lodi na Ono na Bondeni kwa Mafundi.

36Walawi wengine, ambao kwao kulikuwa kwa Wayuda, wakakaa kwa Wabenyamini.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania