Mhubiri 4

Mhubiri 4

1Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.

2Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado;[#Ayu 3:17; Mhu 2:17]

3naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.[#Ayu 3:11; Mhu 6:3; Mt 24:19; Lk 23:29]

4Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.

5Mpumbavu huikunja mikono yake,[#Mit 6:10]

Naye hula chakula chake mwenyewe;

6Heri konzi moja pamoja na utulivu,

Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;

na kufukuza upepo.

7Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.

8Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.[#Mit 27:20; Mhu 1:8; Hab 2:5,6; 1 Yoh 2:16; Zab 39:6; Lk 12:20]

Thamani ya kuwa na rafiki

9Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;

Kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao.

10Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kupata moto?

12Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watamstahimili; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

13Heri kijana maskini mwenye hekima

Kuliko mfalme mzee mpumbavu

ambaye hajui tena kupokea maonyo.

14Kwa maana anaweza kutoka gerezani kutawala; hata ikiwa alizaliwa akiwa maskini katika ufalme.

15Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya mfalme.

16Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kufukuza upepo.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya