The chat will start when you send the first message.
1Kisha ikawa, hapo huyo Yabini, mfalme wa Hazori, aliposikia habari ya mambo hayo, akatuma mjumbe aende kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na mfalme wa Akshafu,[#Amu 4:2; Zab 2:1,2; 83:1-18; Yos 10:3; 19:15]
2na hao wafalme waliokuwa upande wa kaskazini, katika nchi ya vilima, na katika Araba upande wa kusini wa Kinerethi, na katika Shefela, na katika nchi tambarare za Dori upande wa magharibi,[#Hes 34:11; Yos 17:11; Amu 1:27; 1 Fal 4:11]
3na kwa Mkanaani upande wa mashariki, na upande wa magharibi, na kwa Mwamori, na Mhiti, na Mperizi na Myebusi katika nchi ya vilima, na kwa Mhivi pale chini ya Hermoni katika nchi ya Mispa.[#Amu 3:3; Yos 13:11; Mwa 31:49; Amu 20:1; 21:5,8; 1 Sam 10:17; 1 Fal 15:22]
4Nao wakatoka nje, wao na mjeshi yao yote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana.[#Mwa 22:17; 32:12; Amu 7:12; 1 Sam 13:5]
5Wafalme hao wote wakakutana pamoja; wakaenda na kupanga mahema yao pamoja hapo penye maji ya Meromu, ili kupigana na Israeli.
6BWANA akamwambia Yoshua, Wewe usiogope kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa wakiwa wameuawa wote mbele ya Israeli; utawakata farasi wao, na magari yao utayateketeza kwa moto.
7Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafla; wakawashambulia.
8BWANA akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza mpaka kufikia Sidoni ulio mkuu, tena hadi kufika Misrefoth-maimu, tena hata kufikia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawaua wote, wasibakize hata mtu mmoja
9Yoshua akawafanyia vile vile kama BWANA alivyomwamuru; akawakata farasi wao, na kuteketeza magari yao kwa moto.
10Yoshua akarudi wakati huo na kuutwaa Hazori, akampiga mfalme wa Hazori kwa upanga; kwa kuwa Hazori hapo awali ulikuwa ni kichwa cha falme hizo zote.
11Nao wakawapiga wote pia waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa; hakubakizwa hata mmoja akiwa hai; kisha akauteketeza Hazori kwa moto.
12Tena miji yote ya wafalme hao, na wafalme wake wote, Yoshua akawatwaa, akawapiga kwa makali ya upanga, na kuwaangamiza kabisa; vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyomwamuru.[#Hes 33:52; Kum 7:2; 20:16,17]
13Lakini katika habari ya miji hiyo iliyosimama katika vilima vyao, Israeli hakuteketeza kwa moto miji hiyo, isipokuwa ni mji wa Hazori tu; mji huo Yoshua aliuteketeza kwa moto.
14Tena nyara zote za miji hiyo, na wanyama wa miji, wana wa Israeli walitwaa kuwa nyara zao wenyewe; lakini kila mtu wakampiga kwa makali ya upanga, hadi walipokuwa wamewaangamiza wote, wala hawakumsaza mmoja mwenye kuvuta pumzi.
15Vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa mtumishi wake, ndivyo Musa alivyomwamuru Yoshua; naye Yoshua akafanya hivyo; hakukosa kufanya neno lolote katika hayo yote BWANA aliyomwamuru Musa.[#Kut 34:11; Kum 7:2; Yos 1:7]
16Hivyo Yoshua akatwaa nchi hiyo yote, hiyo nchi ya vilima, na nchi yote ya Negebu, na nchi yote ya Gosheni, na hiyo Shefela, na hiyo Araba na nchi ya vilima vilima ya Israeli, na hiyo nchi tambarare;[#Yos 12:8; 10:41]
17tangu kilima cha Halaki, kiendeleacho upande wa Seiri, mpaka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni chini ya kilima cha Hermoni; naye akawatwaa wafalme wao wote, akawapiga, na kuwaua.[#Yos 12:7; Kum 7:24]
18Yoshua akapiga vita siku nyingi na wafalme hao wote.
19Haukuwapo mji hata mmoja uliofanya amani na wana wa Israeli, isipokuwa ni wale Wahivi waliokaa Gibeoni; wakaitwaa yote kwa vita.[#Yos 9:3,7]
20Kwa kuwa lilikuwa ni la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.[#Kum 7:16; Kut 4:21; Kum 2:30; Amu 14:4; 1 Sam 2:25; 1 Fal 12:15; 22:20-23; Rum 9:18; Yak 1:13-17; Kum 20:16]
21Wakati huo Yoshua akaenda na kuwakatilia mbali hao Waanaki watoke nchi ya vilima, kutoka Hebroni, na kutoka Debiri, na kutoka Anabu, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Yuda, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Israeli; Yoshua akawaangamiza kabisa na miji yao.[#Hes 13:22; Kum 1:28; 2:21; Yos 15:13,14; Amu 1:10; Yer 3:23]
22Hawakusalia Waanaki hata mmoja katika nchi ya wana wa Israeli; isipokuwa walisalia katika Gaza, na katika Gathi, na katika Ashdodi.[#1 Sam 17:4; Yos 15:46]
23Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa makabila yao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.[#Hes 34:2; 26:53; Yos 14:15; 21:44; 23:1]