Yoshua 12

Yoshua 12

Wafalme walioshindwa na Musa

1Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;[#Hes 21:21-35; Kum 2:26—3:11; Amu 11:18; Isa 16:2; Kum 3:8,9]

2Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hadi kuufikia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;

3na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Araba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya materemko ya Pisga;[#Kum 3:17; Yos 13:20]

4tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,[#Hes 21:35; Kum 3:11]

5naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hadi mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni.[#Yos 13:11; Kum 3:14; 1 Sam 27:8; 2 Sam 3:3; 13:37; 2 Fal 25:23]

6Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase iwe urithi wao.[#Hes 32:33; Kum 3:12]

7Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa makabila ya Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao;[#Mwa 14:6; 32:3]

8katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika materemko, na katika nyika, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;[#Kut 3:8; Yos 10:40]

9mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja;[#Yos 6:2; 8:29]

10mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja;[#Yos 10:23]

11mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja;

12mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja;

13mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja;

14mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja;

15mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;

16mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja;

17mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja;[#Yos 19:13; 1 Fal 4:10]

18mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja;[#Isa 33:9]

19mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja;

20mfalme wa Shimron-meroni, mmoja; na mfalme wa Akshafu, mmoja;[#Yos 11:1; 19:15]

21mfalme wa Taanaki, mmoja; na mfalme wa Megido, mmoja;

22na mfalme wa Kedeshi, mmoja; mfalme wa Yokneamu wa Karmeli, mmoja;[#Yos 19:37]

23mfalme wa Dori katika kilima cha Dori, mmoja; na mfalme wa makabila katika Gilgali, mmoja;[#Mwa 14:1,2; Isa 9:1]

24na mfalme wa Tirza, mmoja; wafalme hao wote walikuwa ni thelathini na mmoja.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya