The chat will start when you send the first message.
1Haleluya.
Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,
Lisifuni jina la BWANA.
2Jina la BWANA lihimidiwe[#Dan 2:20]
Tangu leo na hata milele.
3Toka maawio ya jua hata machweo yake[#Isa 59:19; Hab 2:14; Mal 1:11; Ufu 11:15]
Jina la BWANA husifiwa.
4BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5Ni nani aliye mfano wa BWANA,
Mungu wetu aketiye juu;
6Anyenyekeaye kutazama,[#Isa 57:15]
Mbinguni na duniani?
7Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,[#1 Sam 2:8; Isa 26:19; Dan 12:2]
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8Ili amketishe pamoja na wakuu,[#Ayu 36:7]
Pamoja na wakuu wa watu wake.
9Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,[#1 Sam 2:5; Gal 4:27]
Awe mama ya watoto mwenye furaha.