The chat will start when you send the first message.
1BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni,[#Mdo 12:9]
Tulikuwa kama waotao ndoto.
2Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,[#Ayu 8:21]
Na ulimi wetu kelele za furaha.
Ndipo waliposema katika mataifa,
BWANA amewatendea mambo makuu.
3BWANA alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi.
4Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa,
Kama vijito vya Kusini.
5Wapandao kwa machozi[#Isa 12:1-3; Yer 31:9; Yoe 2:17; Mt 5:4; 2 Kor 7:8-11]
Watavuna kwa kelele za furaha.
6Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.