Zaburi 15

Zaburi 15

Nani atakaa katika patakatifu pa Mungu?

1BWANA, ni nani atakayekaa[#Zab 2:5]

Katika hema yako?

Ni nani atakayeishi

Katika kilima chako kitakatifu?

2Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,[#Zab 84:11; Isa 33:15,16]

Na kutenda haki.

Asemaye kweli kwa moyo wake,

3Asiyesingizia kwa ulimi wake.

Wala kumtenda mwenziwe mabaya,

Wala kumsengenya jirani yake.

4Anayedharau waovu Machoni pake,[#Yos 9:18-20]

Bali huwaheshimu wamchao BWANA

Aliyeapa ingawa kwa hasara yake,

Hayabadili maneno yake.

5Asiyetoa fedha yake apate kula riba,[#Eze 18:8,9]

Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia.

Mtu atendaye mambo hayo

Hataondoshwa milele.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya