Zaburi 60

Zaburi 60

Sala ya ushindi wa kitaifa baada ya kushindwa

1Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,

Umekuwa na hasira, uturudishe tena.

2Umeitetemesha nchi na kuipasua,

Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.

3Umewaonesha watu wako mazito,

Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.

4Umewapa wakuogopao bendera,[#Isa 11:10]

Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.

5Ili wapenzi wako waopolewe,[#Zab 108:6]

Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.

6Mungu amenena kwa utakatifu wake,[#Zab 89:35; Mwa 12:6; Yos 13:27]

Nami nikishangilia.

Nitaigawanya Shekemu,

Na kulipima bonde la Sukothi.

7Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,[#Kum 33:17; Mwa 49:10]

Na Efraimu ni kinga ya kichwa changu.

Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

8Moabu ni bakuli langu la kunawia.

Nitamtupia Edomu kiatu changu,

Na kumpigia Filisti kelele za vita.

9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma?

Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?

10Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?[#Zab 44:9]

Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?

11Utuletee msaada juu ya mtesi,

Maana wokovu wa binadamu haufai kitu.

12Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,[#1 Nya 19:13]

Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya