The chat will start when you send the first message.
1MSIWE waalimu wengi, ndugu zangu, mkijua ya kuwa tutapata hukumu kubwa zaidi.
2Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
3Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, illi watutii, na twageuza mwili wao wote.
4Kaziangalieni merikebu; ingawa ni kubwua namna gani, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote aazimuko kwenda yule aongozae.
5Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, na hujivuna majivuno makuu.
6Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum.
7Maana killa aina ya nyama, na ya ndege, na ya nyama watambaao, na ya vitu vilivyo baharini vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wana Adamu.
8Bali ulimi hapana mwana Adamu awezae kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wana Adamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, mambo haya hayapasi kuwa hivyo.
11Je! chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12Ndugu zangu, mtini waweza kuzaa mazeituni au mzabibu tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na niaji matamu.
13Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
14Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli.
15Hekima hii siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na ya Shetani,
16maana hapo palipo wivu na magomvi, ndipo palipo machafuko, na killa tendo la aibu.
17Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;
18na tunda la baki hupandwa katika amani kwa wale wafanyao amani.