The chat will start when you send the first message.
1HAYA bassi, enyi matajiri! lieni yowe kwa sababu ya mashaka yanayokujieni.
2Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.
3Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itakushuhudieni, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho.
4Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, uliozuiliwa nanyi kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa Sabaoth.
5Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.
6Mmemhukumu mwenye haki mkamwua: nae hashindani nanyi.
7Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
8Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.
9Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
10Watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.
11Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.
12Lakini zaidi ya yote, ndugu, msiape kiapo cho chote, kwa mbingu wala kwa inchi; bali ndio yenu iwe ndio, na sio yenu iwe sio, msije mkaangukia hukumu.
13Mtu wa kwenn amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi.
14Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa wakamwombee, wakimpaka mafuta kwa jina la Bwana.
15Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa.
16Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
17Eliya alikuwa mwana Adamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye: na mvua haikunya juu ya inchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
18Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, inchi ikazaa matunda yake.
19Ndugu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali ya kweli, na mtu mwingine akamrejeza;
20ajue va kuwa veve amrejezae mwenye dhambi, atoke katika njia ya upotovu, ataiokoa roho ya mtu yule na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.