The chat will start when you send the first message.
1NDUGU, nia njema ya moyo wangu, na dua yangu niombayo Mungu kwa ajili ya Waisraeli ndio bii, waokolewe.
2Kwa maana nawashuhudia kwamba wana wivu kwa ajili ya Mungu, lakini hauna msingi wa maarifa.
3Kwa maana, wakiwa hawajui haki ya Mungu, na wakitaka kuithubutisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.
4Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki.
5Kwa maana Musa aieleza haki itokayo kwa sharia, akiandika ya kuwa, Mtu afanyae haya ataishi kwa haya.
6Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakaepanda mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini,)
7au, Ni nani atakaeshuka kuzimuni? (yaani, ni kuleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.)
8Lakini yasemaje? Lile neno ni karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani ni lile neno la imani tulikhubirilo;
9kwa sababu, ukimkiri Kristo Yesu kwa kinywa chako, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua, utaokoka;
10kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu.
11Kwa maana andiko lanena, Killa amwaminiye hatatahayarika.
12Kwa maana hapana tofanti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri wa kufaa watu wote wamwitiao;
13kwa kuwa killa atakaemwita Bwana kwa Jina lake ataokoka.
14Bassi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mkhubiri?
15Tena wakhubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri namna gani miguu yao wakhubirio khabari ya mema.
16Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?
17Bassi imani, chanzo chake ni kusikla; na kusikia kunakuja kwa neno la Mungu.
18Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia,
Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote,
Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu.
19Lakini nasema, Israeli hakufahamu? Hapo kwanza Musa anena,
Nitawatieni moyo wa bidii kwa watu wasio taifa,
Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhabisha.
20Na Isaya ana ujasiri mwingi, anasema,
Nalipatikana nao wasionitafuta,
Nalidhihirika kwao wasioniulizia.
21Lakini kwa israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na ubishi.