Warumi 3

Warumi 3

1BASSI Myahudi ana ziada gani? na kutahiriwa kwafaa nini?

2Kwafaa sana kwa killa njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

3Ni nini, bassi, ikiwa hawakuamini wengine? Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?

4Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na killa mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,

Illi upewe haki katika maneno yako,

Ukashinde uingiapo katika hukumu.

5Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)

6Hasha! kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?

7Kwa maana, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kwa sababu ya uwongo wangu hatta akapata utukufu, mbona mimi nami ningali nikihukumiwa kama ni mwenye dhambi?

8Kwa maana tusiseme (kama tulivyosingiziwa nakama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba sisi twanena), Na tufanye mabaya, illa yaje mema? kuhukumiwa kwao kuna haki.

9Ni nini bassi? Tu bora kuliko wengine? Hatta kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba wote pia wa chini ya dhambi;

10kama ilivyoandikwa, ya kama,

Hakuna mwenye haki hatta mmoja.

11Hakuna afahamuye,

Hakuna amtafutae Mungu.

12Wote wamepotoka, wameoza wote pia;

Hakuna mtenda mema hatta mmoja:

13Koo lao kaburi wazi,

Kwa ndimi zao wametumia hila,

Sumu ya pili ni chini ya midomo yao.

14Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.

15Miguu yao ina mbio kumwaga damu.

16Uharibifu na mashaka njiani mwao.

17Na njia ya amani hawakuijua.

18Kumwogopa Muungu hakuwi machoni pao.

19Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:

20kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.

21Sasa, lakini, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sharia, inashuhudiwa na torati na manabii,

22ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.

23Maana hapana tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, wanaona kwamba wamepungukiwii utukufu wa Mungu:

24wanapewa haki burre kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Yesu Kristo:

25ambae Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa damu yake, kwa njia ya imani, illi aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizotangulia, katika uvumilivu wa Mungu:

26illi aonyeshe haki yake wakati huu, awe mwenye baki na mwenye kumpa haki yeye aaminiye kwa Yesu.

27Ku wapi, bassi, kujisifu? Knmefungiwa mlango. Kwa sharia ya namna gani? Kwa sharia ya matendo? La! bali kwa sharia ya imani.

28Bassi, twahasibu ya kuwa mwana Adamu hupewa baki kwa imani pasipo matendo ya sharia.

29Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa mataifa pia? Naam, wa mataifa pia;

30kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.

31Bassi, je! twaibatilisha sharia kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithubutisha sharia.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania