The chat will start when you send the first message.
1Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi;
mimi si mtu wa majivuno.
Sijishughulishi na mambo makuu,
au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
2Ila nafsi yangu imetulia na kuwa na amani,
kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake;
ndivyo nafsi yangu ilivyo tulivu.
3Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu,
tangu sasa na hata milele.