The chat will start when you send the first message.
1Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na waalimu; miongoni mwao wakiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.[#13:1 Taz Mate 11:19 maelezo.; #13:1 Herode Antipa (taz Luka 3:1).]
2Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”
3Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono, wakawaacha waende zao.[#13:2-3 Taz Mate 6:6 maelezo.]
4Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.[#13:4 Bandari ambayo ililisha mji wa Antiokia.; #13:4 Kisiwa cha Mediteranea.]
5Walipofika Salami walihubiri neno la Mungu katika masunagogi ya Kiyahudi. Yohane alikuwa msaidizi wao.[#13:5 Yohane Marko (Mate 12:12,25; 13:13; 15:37-38), mwenzi wa kazi wa Barnaba (Kol 4:10).]
6Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo, upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Bar-yesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.[#13:6 Jina lenye maana ya au . Wakati huo wanaume wengi wa Kiyahudi waliitwa jina Yoshua (katika Kigiriki ni “Yesu”). Kukutana kwa Paulo na huyo mchawi hapa (aya 6-11) kunafanana na kukutana kwa Petro na yule mchawi wa Mate 8:9-24.]
7Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
8Lakini huyo mchawi Elima, (kama alivyokuwa anaitwa kwa Kigiriki), alijaribu kuwapinga ili kumzuia huyo mkuu wa kisiwa asije akaigeukia imani ya Kikristo.
9Basi, Saulo ambaye aliitwa pia Paulo, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alimkodolea macho huyo mchawi,
10akasema, “Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli; hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka.[#13:10 Huenda hiyo ilikuwa namna ya Paulo ya kusema kwamba huyo Elima, kutokana na matendo yake ya udanganyifu, alifanana na Ibilisi.]
11Sasa, mkono wa Bwana utakuadhibu: utakuwa kipofu na hutaweza kuuona mwanga wa jua kwa kitambo.” Mara kila kitu kikawa kama ukungu na giza kwake, akaanza kwenda huku na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono amwongoze.
12Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa mwaamini; akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.
13Kutoka Pafo, Paulo na wenzake walipanda meli wakaenda hadi Perga katika Pamfulia; lakini Yohane aliwaacha, akarudi Yerusalemu.[#13:13-14 Mji katika mkoa wa Kiroma wa Pamfulia.]
14Lakini wao waliendelea na safari toka Perga hadi mjini Antiokia Pisidia. Siku ya Sabato waliingia ndani ya sunagogi, wakakaa.[#13:14 Tofauti na Antiokia ya Siria. Ling na Luka 4:16-28.]
15Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”[#13:15 Kama desturi, katika Sunagogi watu walisoma sehemu kutoka vitabu vya Mose (Sheria au Pentateuko) na sehemu nyingine kutoka mojawapo ya vitabu vya manabii.]
16Basi, Paulo alisimama, akatoa ishara kwa mkono, akaanza kuongea: “Wananchi wa Israeli na wengine wote mnaomcha Mungu, sikilizeni!
17Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua babu zetu; aliwafanya watu hawa wawe taifa kubwa walipokuwa ugenini kule Misri. Mungu aliwatoa huko kwa uwezo wake mkuu.
18Aliwavumilia kwa muda wa miaka arubaini kule jangwani.[#13:17-18 Baadhi ya hati za mkono zina:]
19Aliyaangamiza mataifa saba ya nchi ya Kanaani akawapa hao watu wake ile nchi kuwa mali yao.[#13:19 Yanatajwa katika Kumb 7:1.]
20Miaka 450 ilipita, halafu akawapatia waamuzi wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samueli.[#13:20 Idadi ya jumla ambayo huenda inajumuisha miaka 400 ya kukaa kule Misri (Mwa 15:13) pamoja na miaka arubaini ya kusafiri jangwani (Kumb 2:7).]
21Hapo wakapendelea kuwa na mfalme, na Mungu akawapa Shauli, mtoto wa Kishi wa kabila la Benyamini, awe mfalme wao kwa muda wa miaka arubaini.[#13:21 1Sam 10:20-21,24. Muda wa ufalme wa Saulo hausemwi kwa yakini katika A.K. yaweza kuwa idadi ya jumla tu.]
22Baada ya kumwondoa Shauli, Mungu alimteua Daudi kuwa mfalme wao. Mungu alionesha kibali chake kwake akisema: ‘Nimemwona Daudi mtoto wa Yese; ni mtu anayepatana na moyo wangu; mtu ambaye atatimiza yale yote ninayotaka kuyatenda.’
23Kutokana na ukoo wake mtu huyu, Mungu, kama alivyoahidi, amewapelekea watu wa Israeli Mwokozi, ndiye Yesu.
24Kabla ya kuja kwake Yesu, Yohane alimtangulia akiwahubiria watu wote wa Israeli kwamba ni lazima watubu na kubatizwa.
25Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wake aliwaambia watu: ‘Mnadhani mimi ni nani? Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakuja baada yangu na mimi sistahili hata kuzifungua kamba za viatu vyake.’
26“Ndugu, nyinyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
27Kwa maana wenyeji wa Yerusalemu na wakuu wao hawakumtambua yeye kuwa Mwokozi, wala hawakuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato. Hata hivyo, waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwa kumhukumu Yesu adhabu ya kifo.
28Ingawa hawakumpata na hatia inayostahili auawe, walimwomba Pilato amhukumu auawe.
29Na baada ya kutekeleza yote yaliyokuwa yameandikwa kumhusu yeye, walimshusha kutoka msalabani, wakamweka kaburini.
30Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu.
31Naye, kwa siku nyingi, aliwatokea wale waliofuatana naye kutoka Galilaya mpaka Yerusalemu. Hao ndio walio sasa mashahidi wake kwa watu wa Israeli.
32Nasi tumekuja hapa kuwaleteeni Habari Njema: jambo lile Mungu alilowaahidia babu zetu,
33amelitimiza sasa kwa ajili yetu sisi wajukuu wao kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu. Kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili:
‘Wewe ni Mwanangu,
mimi leo nimekuwa baba yako.’
34Na juu ya kumfufua kutoka kwa wafu, asipate tena kurudi huko na kuoza, Mungu alisema hivi:
‘Nitakupa baraka takatifu na za kweli nilizomwahidia Daudi.’
35Naam, na katika sehemu nyingine za Zaburi asema:
‘Hutamwacha Mtakatifu wako aoze.’
36Sasa, Daudi mwenyewe alitimiza matakwa ya Mungu wakati wake; kisha akafa na kuzikwa karibu na wazee wake, na mwili wake ukaoza.
37Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka wafu hakupata kuoza.
38Kwa hiyo, jueni, ndugu zangu, kwamba kwa njia ya mtu huyu ujumbe kuhusu kusamehewa dhambi unahubiriwa kwenu;
39na ya kwamba kila mmoja anayemwamini Yesu anasamehewa dhambi zote, jambo ambalo halingewezekana kwa njia ya sheria.
40Jihadharini basi, msije mkapatwa na yale yaliyosemwa na manabii:
41‘Sikilizeni enyi wenye madharau,
shangaeni mpotee!
Kwa maana kitu ninachofanya sasa, nyakati zenu,
ni kitu ambacho hamtakiamini hata kama mtu akiwaelezeni.’”
42Paulo na Barnaba walipokuwa wanatoka katika lile sunagogi, wale watu waliwaalika waje tena siku ya Sabato iliyofuata, waongee zaidi juu ya mambo hayo.
43Mkutano huo ulipomalizika, Wayahudi wengi na watu wa mataifa mengine waliokuwa wameongokea dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na Barnaba. Hao mitume waliongea nao, wakawatia moyo waendelee kuishi wakitegemea neema ya Mungu.
44Siku ya Sabato iliyofuata, karibu kila mtu katika ule mji alikuja kusikiliza neno la Bwana.
45Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
46Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi, wakasema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu liwafikieni nyinyi kwanza; lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uhai wa milele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine.
47Maana Bwana alituagiza hivi:
‘Nimekuweka wewe uwe mwanga kwa watu wa mataifa,
ili uwaletee watu wokovu pote ulimwenguni.’”
48Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.[#13:48 Ling na Rom 8:29-30 na pia Dan 12:1; Luka 10:20; Fil 4:3; Ufu 13:8; 21:27.]
49Neno la Bwana likaenea kila mahali katika sehemu ile.
50Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo lao.
51Basi, mitume wakayakung'uta mavumbi yaliyokuwa katika miguu yao kama onyo, kisha wakaenda Ikonio.[#13:51 Ling na Mat 10:14; Marko 6:11; Luka 9:5; 10:11.]
52Lakini hao wafuasi walikuwa wamejaa furaha na Roho Mtakatifu.