The chat will start when you send the first message.
1“Haya! Sikilizeni enyi makuhani!
Tegeni sikio, enyi Waisraeli!
Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme!
Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki,
badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa,
mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori.
2Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu.[#5:2 Shimo lililochimbwa na kufunika kama mtego. Viongozi wa dini na serikali wamekuwa mtego kwa watu. Huwakamata na kuwafunga.; #5:2 Yawezekana ni Abeli Shitimu. Ilikuwa katika upande wa mashariki mwa bonde la mdomo wa mlima Yordani. Pia hekalu la Baal-Peori (taz Hes 25:1; Yos 2:1; 3:1).]
Lakini mimi nitawaadhibuni nyote.
3Nawajua watu wa Efraimu,
Waisraeli hawakufichika kwangu.
Nyinyi watu wa Efraimu mmefanya uzinzi,
watu wote wa Israeli wamejitia najisi.
4“Matendo yao yanawazuia wasimrudie Mungu wao.
Mioyoni mwao wamejaa uzinzi;
hawanijui mimi Mwenyezi-Mungu.
5Kiburi cha Waisraeli chaonekana wazi;
watu wa Efraimu watajikwaa katika hatia yao,
nao watu wa Yuda watajikwaa pamoja nao.
6Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe,[#5:6 Taz 4:8,13; Isa 1:11-15; ling 3:5 na 5:15; Amu 5:4. Atakataa matambiko yao na kuwaadhibu. Taz Hos 5:15; Meth 1:28. Ling Yoh 7:34. Mungu alihitaji kutolewa kwa moyo wa kweli sawa na Agano lake. Taz Amo 5:21-22, 6:56; Isa 1:10-17; Yer 7:21-26; pia Meth 21:3.]
kumtafuta Mwenyezi-Mungu;
lakini hawataweza kumpata,
kwa sababu amejitenga nao.
7Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu,[#5:7 Taz maelezo ya 5:3. Pia 1:2; 2:4. Ling Yer 2:27; wamegeukia Mungu.]
wamezaa watoto walio haramu.
Mwezi mwandamo utawaangamiza,
pamoja na mashamba yao.
8“Pigeni baragumu huko Gibea,
na tarumbeta huko Rama.
Pigeni king'ora huko Beth-aveni.
Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!
9Siku nitakapotoa adhabu
Efraimu itakuwa kama jangwa!
Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli,
ni jambo litakalotukia kwa hakika.
10Viongozi wa Yuda wamekuwa
wenye kubadili mipaka ya ardhi.
Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji.
11Efraimu ameteswa,[#5:11 Aya hii maana yake sio dhahiri katika makala ya Kiebrania.]
haki zake zimetwaliwa;
kwani alipania kufuata upuuzi.
12Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu,
kama donda baya kwa watu wa Yuda.
13Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao,
naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao,
watu wa Efraimu walikwenda Ashuru
kuomba msaada kwa mfalme mkuu;
lakini yeye hakuweza kuwatibu,
hakuweza kuponya donda lenu.
14Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu,[#5:14 Vinyago vya wanyama vilivyokuwa vinaabudiwa kama mungu katika Asia ndogo. Taz 13:4-8.]
kama mwanasimba kwa watu wa Yuda.
Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka,
nitawachukua na hakuna atakayewaokoa.
15Nitarudi mahali pangu na kujitenga nao[#5:15 Waisraeli waliamini Mungu anakaa Mlimani Siyoni au hekaluni mwake. Taz Kumb 33 au Zab 18:6; 46:4.; #5:15 Mwenyezi-Mungu atawaacha mikononi mwa adui mpaka wajifunze kisha wamrudie. Taz 10:2; 14:1; ling Zab 63:1; 78:34, pia Amo 2:7,14; 3:5.]
mpaka wakiri kosa lao na kunirudia.
Taabu zao zitawafundisha wanitafute, wakisema: