The chat will start when you send the first message.
1Haya ndiyo maneno aliyotamka nabii Yeremia mnamo mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia naye Baruku mwana wa Neria akawa anayaandika kitabuni.[#45:1 Taz Yer 36:1.]
Yeremia alimwambia Baruku:
2“Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi juu yako wewe Baruku:
3Wewe ulisema, ‘Ole wangu! Mwenyezi-Mungu ameniongezea uchungu juu ya maumivu yangu. Nimechoka kupiga kite, wala sipati pumziko.’
4Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia nikuambie hivi: Tazama, yale niliyojenga nayabomoa, na yale niliyopanda nayang'oa; nitafanya hivyo katika nchi yote.[#45:4 Taz Yer 1:9-10 maelezo.]
5Je, wewe unajitakia mambo makubwamakubwa? Usiyatafute! Achana nayo, maana, ninaleta maangamizi juu ya wanadamu wote. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Wewe tuzo lako ni hili: nitayaokoa maisha yako kila mahali utakapokwenda.”[#45:5 Haisemwi hapa ni mambo gani makubwa ambayo Baruku alikuwa anataka kuyafanya. Lakini wazo lililopo ni dhahiri: Katika hali yenyewe haitafaa kitu kutafuta makubwa; yatosha tu kuokoa maisha yake. Rejea Yer 38:2.]