The chat will start when you send the first message.
1Baada ya mfalme kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, naye Bwana akiwa amempa amani pande zote kutoka kwa adui zake,
2akamwambia nabii Nathani, “Mimi hapa ninaishi katika jumba la kifalme la mwerezi, wakati Sanduku la Mungu limebaki katika hema.”
3Nathani akamjibu mfalme, “Lolote ulilo nalo moyoni, endelea ukalifanye, kwa maana Bwana yu pamoja nawe.”
4Usiku ule neno la Bwana likamjia Nathani, kusema:
17Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.
18Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana , akasema: