The chat will start when you send the first message.
1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza
tulipokumbuka Sayuni.
2Kwenye miti ya huko
tulitundika vinubi vyetu,
3kwa maana huko hao waliotuteka
walitaka tuwaimbie nyimbo;
watesi wetu walidai nyimbo za furaha;
walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja
kati ya nyimbo za Sayuni!”
4Tutaimbaje nyimbo za Mwenyezi Mungu,
tukiwa nchi ya kigeni?
5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu,
basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu
kama sitakukumbuka wewe,
kama nisipokufikiri Yerusalemu
kuwa furaha yangu kubwa.
7Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu,
siku ile Yerusalemu ilipoanguka.
Walisema, “Bomoa, bomoa
hata misingi yake!”
8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,
heri yeye atakayekulipiza wewe
kwa yale uliyotutenda sisi:
9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga
na kuwaponda juu ya miamba.