The chat will start when you send the first message.
1Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,
hakuna hata mmoja atendaye mema.
2Mungu anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu.
3Kila mmoja amegeukia mbali,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja!
4Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti Mungu?
5Hapo waliingiwa na hofu kuu,
ambapo hapakuwa na hofu.
Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia;
uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau.
6Laiti wokovu wa Israeli ungekuja kutoka Sayuni!
Mungu anaporejesha wafungwa wa watu wake,
Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!