Zaburi 67

Zaburi 67

Zaburi 67

Mataifa wahimizwa kumsifu Mungu

1Mungu aturehemu na kutubariki,

na kutuangazia nuru za uso wake,

2ili njia zako zijulikane duniani,

wokovu wako katikati ya mataifa yote.

3Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

mataifa yote na wakusifu.

4Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe,

kwa kuwa unatawala watu kwa haki

na kuongoza mataifa ya dunia.

5Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

mataifa yote na wakusifu.

6Ndipo nchi itatoa mazao yake,

naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

7Mungu atatubariki

na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.