The chat will start when you send the first message.
1Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
kwa maana ametenda mambo ya ajabu;
kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu
umemfanyia wokovu.
2Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane
na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.
3Ameukumbuka upendo wake
na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;
miisho yote ya dunia imeuona
wokovu wa Mungu wetu.
4Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote,
ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
5mwimbieni Bwana kwa kinubi,
kwa kinubi na sauti za kuimba,
6kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:
shangilieni kwa furaha mbele za Bwana , aliye Mfalme.
7Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake,
dunia na wote wanaoishi ndani yake.
8Mito na ipige makofi,
milima na iimbe pamoja kwa furaha,
9vyote na viimbe mbele za Bwana ,
kwa maana yuaja kuhukumu dunia.
Atahukumu dunia kwa haki
na mataifa kwa haki.