Zaburi 125

Zaburi 125

Usalama wa watu wa Mungu

1Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,

Ambao hautikisiki, wakaa milele.

2Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,

Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,

Tangu sasa na hata milele.

3Kwa maana fimbo ya udhalimu

Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki;

Ili wenye haki wasije wakainyosha

Mikono yao kwenye upotovu.

4Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,

Nao walio wanyofu wa moyo.

5Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,[#Mit 2:15; Isa 59:8; Flp 2:15; Gal 6:16]

BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.

Amani ikae na Israeli.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania