Zaburi 149

Zaburi 149

Sifa kwa wema wa Mungu kwa Israeli

1Haleluya.[#Isa 42:10]

Mwimbieni BWANA wimbo mpya,

Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.

2Israeli na amfurahie Yeye aliyemwumba,[#Ayu 35:10; Zek 9:9]

Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.

3Na walisifu jina lake kwa kucheza,

Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.

4Kwa kuwa BWANA amewaridhia watu wake,[#Mit 11:20]

Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

5Watauwa na waushangilie utukufu,

Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.

6Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,[#Kum 7:1-2; Ebr 4:12; Ufu 1:16]

Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.

7Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,

Na adhabu juu ya makabila ya watu.

8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,

Na wakuu wao kwa pingu za chuma.

9Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa;[#Kum 7:1-2; Rum 16:20; 1 Yoh 5:4]

Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.

Haleluya.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania