Zaburi 54

Zaburi 54

Sala ya uthibitisho

1Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe,

Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.

2Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,

Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

3Kwa maana wageni wamenishambulia;

Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;

Hawakumweka Mungu mbele yao.

4Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;[#Zab 118:7; Isa 41:10; Rum 8:31,32; Ebr 13:6]

Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.

5Atawarudishia adui zangu ubaya wao;[#Zab 89:49]

Uwaangamize kwa uaminifu wako.

6Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu;

Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.

7Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu;

Na jicho langu limeridhika

Kwa kuwatazama adui zangu.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania